Thursday, June 12, 2014

MECHI IMEMALIZIKA NA KUFANYA TIMU YA BRAZIL KUIBUKA NA USHINDI DHIDI CROATIA KATIKA KOMBE LA DUNIA 2014


Mpaka mwisho wa mechi Brazil imeweza kuwa chabanga Croatia kwa jumla ya mabao Matatu kwa Moja, Pia Bao la kufutia machozi la Croatia lilifungwa na Mchezaji wa Brazil "Marcelo" baada ya Kujifunga Baada ya Kupigwa na Mchezaji wa Croatia hivyo kufanya kuweza kujiakikishia kuwa na bao lililofungwa katika dakika za mapema ikiwa ni Dkk ya 11.

Bao la Kwanza kwa upande wa Brazil lilifungwa na Mchezaji Mashukhuri yule anayechezea kule Spain katika timu ya Barcelona aitwae "Neymar", bao ilo likifungwa katika Dkk ya 29 kwa mkwaju uliopigwa mita chache kutoka usawa ama nje kidogo ya boksi kubwa.


Bao la pili la Brazil lilifungwa katika Dkk ya 71 kupitia kwa mchezaji wake "Neymar" mfungaji wa Bao la kwanza katika timu ya hiyo lilifungwa kwa mkwaju wa Penalt, baada ya mchezaji wa Brazil kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane.

Pia bao la tatu la Brazil lilifungwa na mchezaji anayechezea kule England "Chelsea" aitwae Oscar baada ya kuwatoka mabeki wa Croatia na hivyo kufanga bao jepesi katika Dkk ya 90 pindi zikisalia dakika chache mpira kuisha.
Hivyo kufanya Brazil kuibuka na Ushindi mnono baada ya kuichalanga Croatia kwa jumla ya Mabao matatu kwa moja 3:1

           Imeandikwa na Repoter KHALEED SALUM

No comments:

Post a Comment