Sunday, June 15, 2014

Soma mashairi ya nyimbo mpya ya amini wa Tht


wimbo;asante
mahadhi;zuku rhumba

verse 1
Zile nyimbo ulosikia sio kama ni idea
ni maisha nilopitia
Wakaribu ndio wanaojua
kila mti niliodandia,kumbe matawi yashajiachia
kazi yangu kukesha na dua, labda kesho ntajaliwa
kwa huruma ukatokea, Maumivu yangu Yalikusumbua
Magazeti Redioni pia ulinisoma na kuniskia, japo majibu niliyatoa imani zao hazikunisahishia
Umekuja kuninasua, usinitege ikajirudia

Ulaya wataka Blatter ajiuzulu kwa usemi

Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa shirikisho la kimataifa la kandanda FIFA, Sepp Blatter, ajuzulu kutokana na madai ya rushwa yanayoindama Fifa.
Maafisa wa kandanda wa Europa sasa 







Wametilia shaka uongozi wake.
Mkuu wa chama cha soka cha uholanzi MichaelVan Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter ,Fifa imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili Fifa kujisafisha ni sharti Blatter angatuke.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka Uingereza, Greg Dyke,amesthtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022 yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa rangi.
Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza Fifa katika uchaguzi wa Fifa unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Kwa sasa wajumbe wa Fifa wanavikao huko Sao Paulowakijiandaa kwa ufunguzi wa kombe la dunia hapo kesho ambako Sepp Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema vibaya Fifa na Qatar.
                                                                  habari na abdul jr

Ivory Coast yan'gara Brazil

Miamba ya soka barani Afrika IvoryCoast imeimarisha matumaini ya bara hili baada ya kutoka nyuma na kuishinda Japan kwa mabao mawili kwa moja.
Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Gervinho huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda.

Ikiwa ni mara ya tatu kwa Ivory Coast kushiriki katika michuano ya Kombe la dunia,haijawahi kufuzu kupitia michuano ya kimakundi.Ushindi huo wa Ivory Coast ni wa kwanza miongoni mwa timu za bara hili na unaiweka timu hiyo sawa kwa pointi na Colombia ambayo iliifunga Ugiriki mabao matatu bila jibu.

Matokeo ya Uingereza na Italy

Mabingwa wa zamani wa kombe la dunia Italy imeanza vyema kampeni yake ya kuwania kombe la dunia nchini Brazil baada ya kuichapa Uingerezamabao mawili kwa moja katika mechi kali









Bao la ushindi la Italy lilifungwa kwa kichwa kupitia mshambuliaji matata Mario Baloteli mda mchache tu baada ya kipindi cha mapumziko.
Mechi hiyo ilichezwa chini ya viwango vya juu vya joto katika uwanja wa Manaus uliopo katikati ya msitu wa Amazon.Awali mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge alikuwa amekomboa bao lililofungwa na Claudio Marchisio wa Italy.

Thursday, June 12, 2014

Naf Beach Hotel na Offer Mpya kwa Wateja wake


NAF Beach Hotel ni Hotel yenye hadhi ya nyota Tano iliyopo mkabala na Chuo cha Veta Mtwara Kwa upande wa Mashariki na Pia katika upande Kaskazini ikipakana na Bahari ya Hindi. Uongozi Wa Naf Beach Hotel unapenda kuwatangazia kuwa kutokana na kuwajali wateja wake wale waingiao ndani ya Mkoa wa

MECHI IMEMALIZIKA NA KUFANYA TIMU YA BRAZIL KUIBUKA NA USHINDI DHIDI CROATIA KATIKA KOMBE LA DUNIA 2014


Mpaka mwisho wa mechi Brazil imeweza kuwa chabanga Croatia kwa jumla ya mabao Matatu kwa Moja, Pia Bao la kufutia machozi la Croatia lilifungwa na Mchezaji wa Brazil "Marcelo" baada ya Kujifunga Baada ya Kupigwa na Mchezaji wa Croatia hivyo kufanya kuweza kujiakikishia kuwa na bao lililofungwa katika dakika za mapema ikiwa ni Dkk ya 11.

Bao la Kwanza kwa upande wa Brazil lilifungwa na Mchezaji Mashukhuri yule anayechezea kule Spain katika timu ya Barcelona aitwae "Neymar", bao ilo likifungwa katika Dkk ya 29 kwa mkwaju uliopigwa mita chache kutoka usawa ama nje kidogo ya boksi kubwa.


Bao la pili la Brazil lilifungwa katika Dkk ya 71 kupitia kwa mchezaji wake "Neymar" mfungaji wa Bao la kwanza katika timu ya hiyo lilifungwa kwa mkwaju wa Penalt, baada ya mchezaji wa Brazil kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane.

Pia bao la tatu la Brazil lilifungwa na mchezaji anayechezea kule England "Chelsea" aitwae Oscar baada ya kuwatoka mabeki wa Croatia na hivyo kufanga bao jepesi katika Dkk ya 90 pindi zikisalia dakika chache mpira kuisha.
Hivyo kufanya Brazil kuibuka na Ushindi mnono baada ya kuichalanga Croatia kwa jumla ya Mabao matatu kwa moja 3:1

           Imeandikwa na Repoter KHALEED SALUM

Fifa imefanya haitabadili utaratibu kuhusu Brazil

Fifa imesema haina mpango wa kuhamisha michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 kutoka nchini Brazil ingawa nchi hiyo imepata changamoto katika maandalizi ya michuano hiyo.
Wafanyakazi wawili walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na nguzo ambazo ziliharibu uwanja wa Corithians ulio mjini Sao Paulo.

Vyanzo vya habari vya juu ndani ya Shirikisho hilo vimeendelea kusisitiza kuwa hakuna mbadala kutokana na kutokea kwa ajali hiyo.Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kucheza mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwa na watazamaji 65,000.

DRC na RWANDA zapigana kwa siku ya 2



Mapigano yameendelea kwa siku ya pili kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wale kutoka Rwandakwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Milio ya risasi iliyodumu karibu saa mbili iliripotiwa kusikika mapema Alhamisi.
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa vikosi vya Rwanda viliingia Mashariki mwa Congo, kumteka nyara na kumuua mwanajeshi wake, huku nayo Rwanda ikisema kuwa wanajeshi wa Congo ndio walioingia nchini mwao na kuwafyatulia risasi.Pande hizo zimekuwa zikishutumiana kwa kuanza mapigano.

Wednesday, June 4, 2014

Platini akanusha alipokea hongo



Makamu wa rais wa FIFA Michel Platini amepinga madai alihongwa
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya ambaye pia ni Makamu wa rais wa FIFA ,Michel Platini amekashifu Gazeti la Daily Telegraph kwa kuashiria kuwa alikutana na aliyekuwa Rais wa shirikisho la bara Asia Mohamed bin Hammam muda mchache kabla ya kura za kuamua mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.
Bin Hammam ambaye kwa sasa amepigwa marufuku ya maisha kwa kushiriki ufisadi ,ana anashtumiwa kwa kuwahonga wanakamati iliwaipigia kura Qatar kuwa mwenyeji 2022.

Brazil yatetea maandalizi yake

Rais Roussef ametetea vikali maandalizi ya kombe la dunia Brazil
Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametetea jinsi ambavyo taifa lake limetayarisha Kombe la Dunia litakaloanza juma lijalo jijini Sao Paulo.
Alisema kuwa michezo hiyo itakuwa yenye ufanisi mkubwa ijapokuwa kumekuwepo na kukosolewa kwa kuchelewa kwa nyanja na miundombinu mbalimbali.
Bi Rousseff ambaye huenda akakumbwa na maandamano mapya ya kupinga serikali, alisema kuwa hawataruhusiwa kuvuruga mashindano hayo.Aliwaambia wanahabari kuwa matatizo ya aina ile ni ya kawaida kila mahali.

Kijue kikosi cha Ufaransa Kombe la Dunia 2014

Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Desichams amekiweka hadharani kikosi chake cha wachezaji 23 kitakachoelekea nchini Brazil, Koha huyo amemjumuisha kikosini kiungo wa Bayarn Munichen Frank Ribery ambaye ametokea katika majeruhi Ufaransa ipo katika kundi E ambapo itapambana na Timu kama Switzland Ecuador na Honduras.

Mechi ya kwanza ya Ufaransa itakua dhidi ya Honduras juni kumi na Tano kikosi hicho cha watu kumi na tatu ni:-
WARINDA LANGO
1. Michael Landreau
2. Hugo Lloris
3. Stephen Ruffier

kisome kikosi cha nigeria kinachoelekea Brazil


baada ya timu mbalimbali za ulaya,afrika na asia zinazoelekeaa kombe la dunia kujumuika na wachezaji ambao walikua kwenye klabu zao kutangaza vikosi mbalimbali ambavyo vinaelekea kombe la dunia nchini brazil.kocha wa nigeria Steven Keshi ametangaza kikosi chake cha majina 23 atakachokitumia

Nigeria-Boko Haram wafanya mauaji



borno iliyoshambuliwa NIgeria
MTWARA NEWZ imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50 zilizopita.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.

Polisi waongezewa mishahara nchini Brazil

Polisi waliandamana wakitaka nyongeza ya mishahara
Serikali ya Brazil inapendekeza kuwapa nyongeza ya asilimia 15.8 mishahara polisi wake ili wasigome wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia wiki ijayo.
Maafisa wakuu wa polisi watapokea nyongeza ya asilimia 12 kuanzia mwezi Julai na nyingine ya asilimia 3.8 mwezi Januari.
Maandalizi ya kombe la dunia ambalo linaanza tarehe 12 Juni, yamekumbwa na maandamano ya kupinga serikali kwa kutumia gharama kubwa kuandaa michuano hiyo.Makubaliano hayo yanakuja baada ya mgomo wa polisi mapema mwaka huu ambapo takriban watu 250,000 walishiriki.