
Kuweka rekodi sawa, PAP ( sio IPTL )
wamelipwa tshs 306 bilioni. Alizosema Rais ni
zile zilizokuwa Benki kama taslimu na dhamana
za Serikali. Ambazo hakusema ni zile ambazo
zililipwa na TANESCO baadaye. Ifahamike
hadidu rejea ( Terms of References ) kwa CAG
kufanya uchunguzi zilitolewa na PAC, hivyo
PAC ndio yenye mamlaka ya kuzisemea,
kuzielezea na kuzitolea ufafanuzi. Kwenye
eneo hili Rais hakuwa sahihi na Ikulu inapasa
kurekebisha. Jumla ya fedha ambayo PAP
wamelipwa kutoka akaunti ya # TegetaEscrow
Ni tshs 306 bilioni.
Muhimu sana
Mamlaka ya Kutafsiri Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali haipo
kwa mkaguliwa ( Serikali ) Bali kwa Bunge.
Bunge hufanya kazi hiyo kupitia Kamati ya
PAC.
JACKSON HALIMOJA
No comments:
Post a Comment